IQNA

Arbaeen na Muqawama

Maqari wa  Iran wasoma Qur’ani  katika Kaburi la Al-Muhandis

23:51 - August 21, 2024
Habari ID: 3479310
IQNA - Kundi la wasomaji Qur’ani (maqari) wa Kiirani walioenda Iraq wakati wa msimu huu wa Arbaeen wameshiriki katika vikao vya  kusoma Qur'ani kwenye kaburi la Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa zamani wa VJeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (PMU).

Abu Mahdi al-Muhandis na kamanda wa zamani wa  Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Luteni Jenerali Qassem Soleimani waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Marekani huko Baghdad, Iraq, Januari 3, 2020.

Kikundi cha Qur'ani cha Dar an-Naeem kiliwasili mjini Najaf siku chache zilizopita na kuandaa duru za kusoma Qur'ani kwenye kaburi tukufu la Imam Ali (AS) na kisha wilayani Mashaya.

Kisha walitembelea kaburi la al-Muhandis kusoma Qur’ani.

Kundi hilo ni sehemu ya Msafara wa Qur’ani wa Arbaeen wa Iran unaojumuisha wataalamu 100 wa Qur'ani wa Iran, maqari na vikundi vya Tawasheeh.

Aidha katika msafara wa Qur’ani kutoka Iran  una maqari 30 bora kutoka nchi tofauti wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa.

Msafara huo unapanga programu mbalimbali za Qur'ani kwa mahujaji nchini Iraq wakati wa msimu wa Arbaeen ya Imam Husseina (AS)

3489584

Kishikizo: arbaeen al muhandis
captcha